Ijumaa 12 Septemba 2025 - 23:50
Shambulizi dhidi ya Qatar ni onyo la tahadhari kwa serikali za Kiislamu/ Mazungumzo yamefichua kuwa nguvu za kigeni za kibeberu ni wavunjaji wa ahadi na madhalimu

Hawza/ Khatibu wa Ijumaa wa Qom amesema: Serikali za Kiislamu, amkeni! Ikiwa hamtasimama, hamtapinga na mkauvua silaha muqawama, nanyi pia mtaathirika; wao wanataka kutoka kwetu eidha kujisalimisha na udhalili au maangamizi.

Kwa mujibu wa mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Alireza A‘rafiy katika khutba za Sala ya Ijumaa tarehe 20 Shahrivar 1404 zilizofanyika katika Musalla Quds Qom, akirejea mwanzo wa mwaka wa masomo wa shule za elimu ya kawaida, vyuo vikuu na hawza za kielimu alisema: Hizi nguzo tatu ni pembetatu yenye nuru, ambayo ufanisi na ustawi wa jamii unategemea ukuaji na ustawi wake. Jamii itakayokuwa na elimu bora, hawza yenye mafanikio na chuo kikuu chenye tija, jamii hiyo itakuwa na mustakbali mwema.

Khatibu wa Ijumaa wa Qom kuhusiana na shambulizi la utawala wa Kizayuni dhidi ya Qatar alisema: Qatar ni nchi yenye muungano na Marekani na ndani yake ipo kambi kubwa ya kijeshi ya Marekani, shambulizi hili, kama sehemu ya mfululizo wa matukio ya miaka hii miwili, limeudhihirisha zaidi uhalisia wa Ubeberu wa Magharibi na utawala wa Kizayuni.

Akasema kwa kusisitiza: Daima ninapigia debe elimu ya kawaida, vyuo vikuu na hawza kwamba kuwafahamu wamagharibi ni jukumu letu. Ndiyo, kuna maendeleo ya kimaada huko Magharibi tunayoyaheshimu, lakini undani wa Magharibi ni mchafu na uovu.

Mkurugenzi wa Hawza za kielimu aliendelea: Imedhihirika kuwa utawala wa Kizayuni unafuatilia ndoto ya “Nile hadi Furat”, zamani wengi hawakuamini, lakini leo wamelitamka wao wenyewe, imedhihirika kuwa utawala wa Kizayuni unafuata fikra potofu za chuki ya kidini na wala siyo wa kidemokrasia-liberali. Imedhihirika kuwa wakati wa mazungumzo huingia sambamba na kushambulia, na ugaidi wa kiserikali na rasmi ndio kauli mbiu yao.

Imam wa Ijumaa wa Qom alikumbusha kuwa: Serikali za Kiislamu, amkeni! Ikiwa hamtasimama, hamtapinga, na mkauvua silaha muqawama, nanyi pia mtaathirika. Wao hawatofautishi mitazamo. Wanataka kutoka kwetu aidha tujisalimishe na tudhalilike au maangamizi. Kukataa mazungumzo, kuuvua silaha muqawama na kukataa kauli mbiu ya dola mbili ni hali halisi ya wazi ambayo leo ipo mbele ya macho ya mataifa.

Mkurugenzi wa Hawza za kielimu nchini alisisitiza: Iran ipo katika mstari thabiti wa muqawama na kusimama imara dhidi ya mashetani wa ulimwengu na utawala wa Kizayuni, kama ilivyokuwa siku za nyuma, kwa uthabiti na maamuzi thabiti.

Taswira ya jamii ya Jahiliyya katika Nahjul-Balagha:

Ayatullah A‘rafiy katika khutba ya kwanza, kwa kuashiria miaka 1500 ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w), alisema: Mtume Mtukufu (s.a.w.) katika umri wa miaka 40 alitumwa, akakaa Makka kwa miaka 13, na katika umri wa miaka 53 akaama.

Akaendelea kusena: Imam Ali (a.s.) katika zaidi ya sehemu 40 ndani ya Nahjul-Balagha amenukuu maneno kuhusu Mtume (s.a.w.w), na katika takriban khutba 10 ametoa taswira ya jamii ya Jahiliyya na zama za Bi‘tha (Utume), na mazingira ya kijamii ambayo ni taswira ya wazi.

Imam wa Ijumaa wa Qom akibainisha kwamba zama kabla ya Bi‘tha zinaitwa zama za Jahiliyya na kwamba kuifahamu mihimili na sababu za kipindi hiki ni funguo muhimu kwa zama zetu, alisema: Maelezo ambayo Amirul-Mu’minin (a.s.) ametoa kuhusu jamii ya Jahiliyya na ulimwengu wa zama za Bi‘tha yanagawanyika katika sehemu mbili. Sehemu ya kwanza ni jamii ya Makka, Madina na Jaziratul-Arab, ambayo imepatiwa nafasi ndogo zaidi.

Akasema kwa kusisitiza: Jaziratul-Arab ilikuwa ardhi yenye historia ndefu na yenye nuru, mahali pa kutumwa Mitume wa Mwenyezi Mungu na ikawa ni chimbuko la kumbukumbu za Ibrahim kipenzi cha Mwenyezi Mungu, hii historia ya kiutamaduni, kimungu na kimaadili ilikuwa yenye thamani, lakini jamii hii katika zama za Bi‘tha ilikuwa katika hali mbaya kabisa yenye kudorora, hakukuwa na dalili yoyote ya ustaarabu, jamii ya kisasa, dola au serikali na wala mfumo wa kijamii, uovu ulikuwa umetanda kiasi kwamba kuabudu masanamu kulikuwa ndio ada, ubaguzi wa kikabila ulikuwa umetawala jamii nzima, na hakukuwa na chochote cha kimaadili, kimaana na kiitikadi cha tauhidi katika kitovu cha tauhidi.

Muujiza wa kwanza wa Uislamu:
Imam wa Ijumaa wa Qom akasema: Kwa upande wa mali pia, hakukuwa na uchumi uliochanua, dola imara, wala nguvu za kijamii na kisiasa za kuzingatiwa. Mtume wa Uislamu kwa chini ya robo karne aliigeuza mazingira haya kuwa jamii yenye maendeleo, dola kinara na nguvu yenye ustaarabu, kiasi kwamba upeo wa mwelekeo wa madhehebu haya ulifika hadi mipaka ya Ulaya na Afrika, kubadilisha mazingira duni kuwa jamii iliyoongoza katika viwango vyote vya kimaada na kimaana ni miongoni mwa miujiza ya Qur’ani na Uislamu.

Akaongeza kusena: Sehemu ya pili ya taswira aliyoitoa Imam Ali (a.s.) kuhusu jamii ya Jahiliyya na ulimwengu wa zama za Bi‘tha haikuhusiana tu na Jaziratul-Arab, bali alitoa maelezo kuhusu dunia yote ya zama za Bi‘tha, makusudio ya Jahiliyya ya zama za Bi‘tha siyo Jaziratul-Arab pekee, bali ilikuwa ni Jahiliyya ya kila upande, ambapo dunia nzima ilikuwa mbali na thamani tukufu, hata nguvu kuu za wakati huo – Rumi na Uajemi – na hata madola madogo zaidi kama India, China, Misri na Habasha pia yalikuwa yamejikita katika kudorora huku.

Khatibu wa Ijumaa wa Qom aliongeza kusem: Imam Aly (as) anasema katika Nahjulbalagha:


«أهلُ الأرضِ (الأرَضینَ) یَومئذٍ مِلَلٌ مُتَفَرِّقَةٌ، وأهواءٌ مُنتَشِرَةٌ، وطَرائقُ (طَوائفُ) مُتَشَتِّتَةً؛»

“Watu wa ardhi katika siku hizo walikuwa na dini zilizotawanyika, matamanio yaliyoenea, na njia (makundi) yaliyogawanyika.
Katika zama hizo, watu wa dunia walifuata dini zilizopotea kila upande, walikuwa na malengo na imani tofauti na walitembea katika njia zilizogawanyika.”

Na katika hotuba nyengine anasema:


«بَعَثَهُ وَ النَّاسُ ضُلَّالٌ فِی حَیْرَةٍ، وَحَاطِبُونَ فِی فِتْنَةٍ، قَدِ اسْتَهْوَتْهُمُ الْأَهْوَاءُ، وَاسْتَزَلَّتْهُمُ الْکِبْرِیَاءُ، وَاسْتَخَفَّتْهُمُ الْجَاهِلِیَّةُ الْجَهْلاَءُ؛»

“Mwenyezi Mungu alimtuma Mtume wakati ambapo watu walikuwa wamepotea katika hali ya kutojua na kuchanganyikiwa; walihangaika ndani ya fitna, matamanio ya nafsi yalikuwa yamewapotosha, kiburi kiliwadidimiza, na jahiliyya ya upumbavu na upotofu ikawafanya kuwa watu wapuuzi na wasio na thamani.”

Kisha Khatibu wa Ijumaa wa Qom akaendelea kusema: Khutba hizi hazikuhusiana tu na Jaziratul-Arab bali zinahusu dunia nzima, Jahiliyya hiyo ipo hata leo, na sasa tunashuhudia jahiliyya ya kisasa katika nguvu za kibeberu za ulimwengu, tukio la Ghaza, vita na dhulma wanazozieneza duniani ni miongoni mwa dalili za kudorora kwao.

Imam wa Ijumaa wa Qom akaongeza kusema: Amirul-Mu’minin (a.s.) kuhusu sifa za zama za jahiliyya anasema kuwa dunia nzima ilikuwa imelala, hata nguvu kubwa nazo zilikuwa ndani ya shirki na kuporomoka kimaadili, dini zilikuwa zimepotoshwa, hakuna utamaduni mtukufu wa kimungu uliokuwepo duniani, giza na ujinga, vita, ta‘asub zisizo na maana, dhulma na ubaguzi, macho yalikuwa yamelala na nyoyo zimefungwa.

Muujiza wa Pili wa Uislamu

Mkurugenzi wa Hawza za kielimu nchini Iranj, akieleza kuwa Mtume (s.a.w.w) aliiamsha jamii iliyolala na kuyafumbua macho yaliyokuwa yamefungwa katika ulimwengu wa ghaibu na tauhidi, alisema: Muujiza wa pili wa Mtume ni kwamba aliuamsha ulimwengu wote uliokuwa umelala katika shirki na utumwa wa Shetani, akauamsha na kuupa zawadi mpya.

Khatibu wa Ijumaa wa Qom akasema: Mtume (s.a.w.w) aliweka msingi wa ustaarabu ambao una ustawi wa kimaada na vilevile umefungua milango mipya ya ghaibu kwa wanadamu, kama siyo Bi‘tha na kuzaliwa kwa Mtume (s.a.w.w), dunia nzima ingeliendelea katika upotevu huo, Mtume ana haki juu ya ulimwengu wote.

Ayatullah A‘rafiy mwishoni alisema: Katika kumbukumbu ya miaka elfu moja na mia tano tangu kuzaliwa kwa Mtume (s.a.w.w), tuboreshe tena ahadi yetu kwake, umma wa Kiislamu unapaswa kumrudia Mtume (s.a.w.w), malezi ya Mtume (s.a.w.w) yanapaswa kuzitia nuru nyoyo zetu, kuziunganisha nyoyo zetu pamoja, kuzipanga safu za umma wa Kiislamu na kulitia nguvu jeshi la tauhidi.
 

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha